Hii si Shule ya Kawaida
Shule ya kisasa inayokuja mtaani kwako β kwa kutumia nyumba za wazazi kama madarasa (ThinkPods) na wawezeshaji wanaoitwa Creative Mentors.
πKwa watoto wa miaka 7β14 | π§ Wiki 4-6 za kusisimua | π ThinkPod moja, ubunifu mwingi
π Mpango wa majaribio (Pilot Program) umeanza! Jiunge nasi sasa kabla nafasi hazijaisha.
Shule Ilipoishia, ThinkShule Inaanzia
Watoto wengi wanafundishwa kukariri. Wachache wanafundishwa kufikiri, kutatua, kubuni au kuuliza kwanini.
Hapa ndipo ThinkShule inapoingia kati.
ThinkShule ni harakati mpya ya elimu nchini Tanzania β shule iliyowekwa kwenye mtaa, ndani ya familia na katika mioyo ya watoto. Tunabadilisha mfumo tukilenga fikra, siyo ukariri.
Elimu iliyotengenezwa kwa maisha halisi ya kitanzania na Afrika, tukilenga kubadilisha nyumba moja baada ya nyingine, mtaa mmoja baada ya mwengine kupitia;
- π§ Ubunifu Kwanza
- π‘ Darasa la Nyumbani
- π Watoto Huru Kufikiri
- π€ Jamii Inayoshirikiana
Misheni Yetu
ThinkShule hatufundishi kukariri na kujibu mitihani kama shule zingine. Tunafundisha kufikiri, kutatua, kujieleza na ubunifu sahihi ndani ya ThinkPods. ThinkPods ni madarasa ya mtaa kwenye nyumba salama za wazazi waliochaguliwa. Hakuna sare. Hakuna madawati. Ni elimu ya kweli pale maisha yanapoishi.
Hatuoni elimu kama ngazi. Bali tunaiona kama karakana (workshop) β tukiwa na zana, maswali, kujaribu na cheche za kibunifu.
Tunaamini Nini?
Watoto si tu wanafunzi β ni wavumbuzi, wabunifu na viongozi wa kesho.
ThinkShule inaleta elimu ya mazoezi, fikra bunifu, ujasiriamali na uongozi moja kwa moja katika mazingira ya nyumbani kwa kutumia njia rahisi, ya karibu na yenye mvuto kwa watoto.
Programu Zetu
- ThinkShule Weekend (Jumamosi & Jumapili β Wiki 6)
β° Kwa wakati wa shule
π Vipindi vya dakika 90β120 kila wikiendi
π― Mada za ubunifu, changamoto, kujieleza (storytelling) na kushirikiana (teamwork)
π Zinafanyika kwenye ThinkPods ndani ya mtaa wako
π Sajili Mtoto Wako
- ThinkShule Holiday (Kipindi cha Likizo β Wiki 4)
β° Kwa wakati wa likizo ya shule
π Vipindi mara 2β3 kwa wiki kulingana na ratiba ya pod
π Watoto hupata muda zaidi, uzoefu mkubwa kwa kipindi kifupi
π Huduma hii huleta matokeo makubwa (maximum impact) kwa likizo nzima
Kutana na Mwanzilishi wa ThinkShule

ThinkShule imeanzishwa na Shamte Kilalile, muwezeshaji (mentor) wa kitanzania, mfikiliaji na muundaji wa mifumo (systems thinker & builder). Kabla ya ThinkShule, Shamte alianzisha programu ya Very Good Tutors (VGT), kupitia VGT alijifunza nini kinatokea ikiwa mfumo haujajaribiwa vyema. Mara hii kupitia ThinkShule anaanzia chini kutoka kwenye jamii na mpango wa majaribio (Pilot program) kabla hajaamua kuendeleza (scale up). Anapatikana sana mtandao wa LinkedIn akiongea kuhusu AI, kuunda mifumo kwa biashara za kiafrika na mengine mengi.
Jinsi ThinkShule Inavyofanya Kazi
Programu zetu zina hatua zifuatazo;
Hatua ya 1: Tunawakusanya watoto kwenye ThinkPods
Kila ThinkPod moja ina watoto 3-10 (umri 7β14). Wanakutana kwenye nyumba moja tuliyoichagua kwa kuwa imefikia vigezo vyetu. Nyumba hii ni ya mzazi na ndio mwenyeji wetu katika mtaa husika.
Bonasi: kama utaifanya nyumba yako kuwa ThinkPod yetu,
- mtoto wako mmoja ataingia kwenye programu yetu bure,
- mtoto wa pili na kuendelea utapata punguzo la 10%
- ahsante kwa kuwa partner wetu ya Shilingi 15,000
- utapata TZS 5,000 kwa kila mtoto wa jirani yako utakayemshawishi kujiunga nasi
Unayo nafasi ya kuigeuza nyumba yako kuwa ThinkPod β kitovu cha mafunzo kwa watoto wa mtaa wako?
π Weka Nyumba Yako Iwe ThinkPod
Hatua ya 2: Kujifunza kwa Vitendo
Kila wiki ina maudhui (theme) β sio somo. Maudhui yaweza yakawa:
- βMaabara ya Kutatuaβ (tunafundisha kutatua changamoto)
- βTaka kuwa Dhahabuβ (kujua fursa iliyojificha katika vitu vinavyoonekana duni)
- βMbunifu wa Mtaaβ (kutengeneza kitu cha kibunifu kwa rasilimali rahisi zinazopatikana kwenye mazingira yetu)
Hatuna mitihani. Hatuna sare za shule. Ni zana, mawazo na kutaka kujua kwanini.
Watoto watatengeneza, kudizaini, kufikiri sio kusikiliza na kukariri tu wakiongozwa na muwezeshaji wetu (Creative Mentor). Hawa sio walimu wa kawaida β hawa ni vijana wabunifu, wanaopenda kusaidia watoto kuchimbua kile kilichopo ndani yao. Wanaandaliwa na ThinkShule na wanatoa uzoefu usiosahaulika.
Tunawakaribisha vijana wabunifu, walimu, wahitimu na wale walio na moyo wa kuwalea watoto kiubunifu. Unapokuwa muwezeshaji wetu (Creative Mentor), unapata:
- Nafasi ya kuleta mabadiliko (impact) kwenye kizazi kijacho
- Mafunzo maalum kabla ya kuanza
- Miongozo ya kila session
- Posho kwa kila ThinkPod utakayoiendesha
π Jisajili Kama Creative Mentor
Hatua ya 3: Tunakutana kwa vipindi 2-3 kwa wiki
Kila kipindi ni takribani masaa 1.5-2.
Kila ThinkPod ina:
- Vipindi 2 vya kujadili na kudizaini/kutengeneza
- Kipindi 1 cha wazazi kuhudhuria maonyesho ya watoto wao.
Hatua ya 4: Kuhitimisha Wiki ya 4 au 6
Kila ThinkPod ina safari ya wiki 4 (kwa ThinkShule Holiday) au wiki 6 (ThinkShule Weekend). Miwsho wa kila programu:
- Watoto watawasilisha walivyovitengeneza
- Wazazi wataona mabadiliko ya ukuaji kabla na baada ya programu
- Cheti kitapatikana kutegemea na kifurushi cha gharama atakachochagua mzazi kwa ajili ya mwanae. Soma bei zetu .
- Baada ya programu hii ya majaribio unaweza kujiunga na programu rasmi tukiianzisha
Bei Zetu
Bei rafiki kwa kila mzazi wa mtoto:
π± Kifurushi cha Basic Thinker β TZS 60,000
- Mtoto anahudhuria wiki zote 4 (ThinkShule Holiday) au wiki 6 (ThinkShule Weekend)
- Kazi binafsi na kikundi
- Fursa ya kuonyesha alichokifanya mwisho wa programu (End-of-program showcase)
π Kifurushi cha Explorer Tier β TZS 75,000
- Kila kitu kwenye kifurushi cha Basic Thinker
- Ripoti maalumu ya mrejesho toka kwetu kwenda kwa mzazi kuhusu mtoto wake (Personalized project feedback)
- Cheti mwisho wa programu
π§ Kifurushi cha Premium Parent β TZS 90,000
- Kila kitu kwenye kifurushi cha Explorer Tier
- Ripoti ya kila maudhui ya kila wiki + picha/video za nini mtoto wake amefanya katika maudhui hizo
π§· Punguzo / Bonasi
Kama unahitaji punguzo au bonasi:
- Ukimuandikisha mtoto wako wa pili na kuendelea: -punguzo la 10%
- Muite rafiki/jirani: unajipatia TZS 5,000 kwa kila mtoto utakayemleta
- Ukijiunga mapema: punguzo la TZS 5,000 ukilipa wiki 1 kabla ya ThinkPod ya mtaani kwako kuanza
Maswali Yanauyoulizwa Sana
SWALI: ThinkShule ni tuisheni (tuition) ya ziada?
JIBU: Hapana. ThinkShule si tuisheni, wala hautufudishi masomo ya shuleni. Sisi tunafungua bongo za kuuliza kwanini na nifanyeje kutatua changamoto, ubunifu na ujasiri kupitia mafunzo ya kivitendo.
SWALI: ThinkShule ni kwa ajili ya nani?
JIBU: ThinkShule ni kwa β Wazazi wanaotaka watoto wao wakue kwa fikra huru β Watoto wenye vipaji vya ubunifu, sayansi, teknolojia, sanaa na biashara β Familia zinazotaka elimu tofauti na shule za kawaida.
SWALI: ThinkShule ni kwa rika gani?
JIBU: Kwa sasa ni watoto wa miaka 7β14. Hii ni sawa na darasa la 1 hadi 7. Baadae tutatanua wigo kwa vijana.
SWALI: Ni lini mafunzo yanafanyika?
JIBU: Kwa programu ya ThinkShule Weekend ni siku za Jumamosi na Jumapili pekee, kwa wiki 6 mfululizo. Na programu ya ThinkShule Holiday (Likizo) ni wiki 4.
SWALI: Mafunzo yanafanyika wapi?
JIBU: Kwa sasa ni Dar es Salaam na yanafanyika kwenye nyumba ya jirani yako mtaani kwako tunazoziita ThinkPods. Haya ni madarasa ya mtaa kwenye nyumba salama za wazazi waliochaguliwa. Wasiliana nasi kuuliza kama ipo moja mtaani kwako au unaweza kuwa wewe wa kwanza kuanzisha. Angalia vigezo vyetu kwenye hii fomu yetu.
SWALI: Naweza kuwa ThinkPods yenu mtaani kwangu?
JIBU: Bila shaka. Mwenyeji wetu wa mtaa unapata fursa ya mtoto wako mmoja kusoma bure, punguzo la 10% kwa mtoto wa pili na kuendelea, TZS 15,000 ya ahsante kutukaribisha mtaani kwa kila msimu ThinkShule itakapoendesha programu zake kwenye nyumba yako na TZS 5,000 kwa kila mtoto wa jirani atakayemshawishi kujiunga nasi kwenye ThinkPod yako (wasizidi watoto 10 kwa ThinkPod moja). Tutakuja kuichunguza nyumba yako kama imekamilisha vigezo vyetu. Ikikidhi, basi unastahiki faida tulizotaja.
SWALI: Ili niwe miongoni mwa ThinkPods zenu ni lazima niwe na nyumba ya vyumba vingapi?
JIBU: Angalau kuwepo chumba kimoja cha wazi, kisafi na chenye nafasi ya watoto 3β10. Angalia vigezo vya ziada kwenye fomu yetu.
SWALI: Nimevutiwa na programu yenu na nina nyumba pia. Naweza kujiandikisha kama muwezeshaji wenu (Creative Mentor) na kufanya nyumba yangu ThinkPod yenu?
JIBU: Bila shaka, hii inakupa faida mara mbili: faida za kuwa mwenyeji wa mtaa (tumezitaja kwenye jibu la moja ya swali yaliyotangulia juu) na posho kama muwezeshaji wetu. Jaza fomu yetu ya kuwa muwezeshaji kama wewe ni mwalimu kitaaluma au kijana mbunifu na unapenda kufundisha watoto na fomu ya ThinkPod kwa ajili ya nyumba yako.
SWALI: ThinkShule ni programu ya kidini au mlengo wa kisiasa?
JIBU: Hapana. Sisi ni ubunifu kwanza, kiafrika zaidi, vipaumbele vyetu ni kuchochea akili ya kidadisi, heshima na kutanguliza jamii mbele. Hatuna kingine. Ukiwa kama mwenyeji wetu, ukibaini muwezeshaji wetu (Creative Mentor) anapandikiza fikra za udini na siasa kwa watoto, tafadhari mripoti kwetu tutachukua hatua dhidi yake ikiwemo kumuondoa kwenye programu zetu zote.
SWALI: Gharama/bei zenu zikoje?
JIBU: Tunatumia ThinkPods za watoto 3-10 ili kufanya gharama ziwe shirikishi na nafuu kwa mzazi. Mfano kifurushi cha TZS 60,000 kwa wiki 6 ina maana kila wiki ni TZS 10,000 tu. Lau kama ingelikuwa tunamfundisha mtoto mmoja mmoja isingekuwa kwa bei hiyo. Gharama zetu zinafidia muda wa muwezeshaji kujiandaa, nauli ya kuja ThinkPod na gharama za kununua rasilimali zitakazotumika kwenye maudhui zetu. Baadae tutakuja kuanzisha ThinkPods za ufadhili (community-sponsored pods) kwa wazazi wasio na uwezo kabisa.
SWALI: Nani anaendesha ThinkPods?
JIBU: Wawezeshaji wetu tunaowaita Creative Mentors. Wapo ambao ni walimu kitaaluma na wengine ni vijana wabunifu. Ila wote wanashirikiana sifa-wanapenda kusaidia watoto kuchimbua kile kilichopo ndani yao na wamefundishwa mtaala wa ThinkShule na muanzilishi wa ThinkShule.
SWALI: Muwezeshaji analipwaje?
JIBU: Kwa sasa ni kiwango maalumu (basic flat rate) cha TZS 60,000 kwa ThinkPod ya watoto 3 jumlisha bonasi ya TZS 5,000 kwa kila mtoto atakayemuandikisha kwenye ThinkPod yake mpaka kufikia kiwango cha watoto kichozidi watoto 10 kwa ThinkPod moja. Mfumo huu umewekwa kuwachalenji wawezeshaji wetu kuwa wabunifu kama kile wanachokifundisha kwa watoto wanaowafundisha.
Angalizo-ikiwa ushawishi wa uandikishwaji wa watoto umetokana na Mwenyeji wa ThinkPod (mzazi) basi TZS 5,000 kwa kila mtoto atalipwa huyo mwenyeji na wewe utabakiwa na basic flat rate kwa sababu ya kufundisha. Uko tayari kwa chalenji hii? Jisajiri
Mawasiliano
π Tuna ThinkPods zinazoanza Dar es Salaam, tunapanua mikoa mingine polepole.
π¬ Email: verygoodtutorstz@gmail.com
π² Simu/WhatsApp: +255718-515321
π Instagram: https://www.instagram.com/thinkshule/
π Linktree: https://linktr.ee/thinkshule
Sauti za Watoto. Nguvu za Mtaa. Ndoto za Taifa.

