close
Nenda kwa yaliyomo

Kabila la Lawi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kabila la Lawi (kwa Kiingereza Levi) ni mojawapo kati ya makabila ya Israeli ambayo kwa jumla ni 12, kutokana na watoto wa kiume 12 wa Yakobo Israeli. Kabila hilo hutazamwa kama uzao wa Lawi. Musa alizaliwa katika kabila hilo.[1]

Ndilo kabila pekee lililoteuliwa na Musa kwa kazi ya ukuhani[2]. Kufuatana na taarifa katika Kitabu cha Kutoka, Musa alifanya azimio hilo baada ya kuona juhudi ya kabila lake wakati wa kuwaondoa wafuasi wa ndama ya dhahabu[3].

Wakati wa kuingia katika nchi ya ahadi, Walawi hawakupewa na Yoshua eneo maalum bali walipewa haki ya kupokea sehemu za sadaka na zaka.

Makuhani wa Israeli walikuwa sehemu ya kabila la Lawi. Hadi leo jina la Lawi kwa umbo la Kizungu "Levi" linapatikana kati ya Wayahudi.

BERJAYA Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kabila la Lawi kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.