Monrovia
| Jiji la Monrovia | |
| Nchi | Liberia |
|---|---|
| Idadi ya wakazi | |
| - Wakazi kwa ujumla | 1,021,762 |


Monrovia ni mji mkuu wa Liberia. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2008, mji huu ulikuwa na wakazi wapatao 1,021,762.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Eneo uliko mji huo mwanzoni liliitwa na mabaharia Wareno Cape Mesurado walipowasilia katika miaka ya 1560. Wakati huo tayari kulikuwa na wakazi wakiishi hapo.
Mji ulianza kujengwa mwaka 1822 na chama cha American Colonization Society ikiwa ni makazi ya watu waliokombolewa toka utumwani nchini Marekani.[1] Jina Monrovia lilitokana na jina la Rais wa Marekani James Monroe.
Watu wa kwanza kuhamia Monrovia toka nchini Marekani waliwasili mwaka 1822 katika Kisiwa cha Sherboro nchini Sierra Leone. Wahamiaji wengi walifariki baada ya kuwasili Monrovia.
Mkutano wa kutunga katiba ya Liberia wa American Colonization Society ulifanyikia Monrovia mwaka 1845.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Uchumi wa Monrovia unategemea zaidi bandari yake na madini ya chuma. Bidhaa kama vile saruji, mafuta, matofali, vigae, samani, na kemikali zinatengenezwa Monrovia.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-05-18. Iliwekwa mnamo 2013-06-02.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Monrovia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |

